Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefunguliwa kesi Mahakamani akituhumiwa kutenda makosa ya jinai.

Makosa hayo yanahusisha mambo mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka ikiwa mojawapo ni suala la kuvamia kituo cha habari cha Clouds Media, Machi 17 mwaka 2017.

Kesi dhidi ya Makonda imewasilishwa Mahakamani na Mawakili wa Kujitegemea na inatarajiwa kuanza kusikilizwa Desemba 3 mwaka huu.

Paul Christian Makonda amehudumu kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kipindi cha uongozi wa Hayati Rais John Pombe Magufuli, na baadae akiachia ngazi ya Kuteuliwa na kwenda kugombea Ubunge jimbo la Kigamboni na hatimaye kukosa kuchaguliwa na wajumbe.

Museven awasili Nchini Tanzania
Omicron ndilo jina la kirusi kipya cha Corona