Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ambaye amepewa jukumu la kuwa Mwenyekiti wa kuongoza Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa (Taifa Stars) kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) amezindua rasmi kamati yenye wajumbe 14 ambapo amewaomba wananchi kuwa kitu kimoja katika kuisapoti timu hiyo.

Amesema kuwa majukumu makubwa 3 watakayoanza nayo Kama kamati ni Kuirudisha timu kwa wananchi, kuweka maandalizi mazuri ya timu na uwezeshaji wa timu.

Aidha RC Makonda amesema kuwa kamati imepanga kukutana na watu wa makundi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini, Wasanii, Wanasiasa, Wamiliki wa Vyombo vya Habari na wadau mbalimbali ili kwa pamoja tuiunge mkono timu ya Taifa.

Amesema kuwa kwa sasa timu ipo katika mikakati ya maandalizi ya Mechi ya mwisho dhidi ya Uganda itakayochezwa Machi 24.

Hata hivyo, kamati hiyo inaongozwa na RC Makonda ambaye ni Mwenyekiti, Katibu wake akiwa ni Mhandisi Hersi Said ambapo Wajumbe wa kamati hiyo ni Mohamed Dewji, Haji Manara, Jerry Muro, Farouk Barhoza, Salim Abdallah, Mohamed Nassor, Patrick Kahemele, Abdallah Bin Kleb, Tedy Mapunda, Philimon Ntaihaja, Farid Nahid na Faraji Asas

Boban amvaa Jerry Murro, 'amenikosea sana'
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 26, 2019