Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaomba wananchi wa Dar es salaam kuwa watulivu kipindi hiki ambapo jeshi la polisi linafanya uchunguzi kubaini aliyehusika na tukio la kupigwa risasi Akwilina.

Makonda amesema wananchi wasiwe wa kwanza kunyoshea wengine vidole na kuwalaumu juu ya tukio hilo kwani bado haijafahamika muhusika ni nani.

Pia amesema kama hukumu inatolewa na Mungu peke yake anaamini kuwa Mungu ndio anajua kwa nini Akwilina ameondoka tarehe 16, Februari 2018.

Hivyo amewaomba wananchi watulie na wawape nafasi jeshi la polisi kufanya majukumu yao ya  uchunguzi mpaka utakapoisha ambapo taarifa kamili juu ya aliyesababisha kifo cha Akwilina itatolewa.

“Jeshi hili la Polisi litatupatia majibu watakapomaliza kazi yake, ombi langu kwenu wananchi wa Dar es Salaam hasa wale ambao hatujawahi kusomea mambo ya uchunguzi na wala hatuyajui tusiwe wa kwanza kunyoosha vidole na kuhukumu kabla hatuja hukumiwa. Mimi najua mtoa hukumu wa kweli ni Mungu na anazo siri zote kwa nini Akwilina ameondoka tarehe 16”, amesema Makonda.

Makonda ameeleza hayo wakati aliposhiriki katika ghafla ya kuaga mwili wa marehemu Akwelina katika chuo cha Taifa cha Usafrishaji (NIT) ili aende kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele huko Mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameitaka familia ya marehemu Akwelina iwe yenye uvumilivu katika kipindi kigumu walichonacho kwa sasa.

DC Kasesela, Asia wafanya ziara Kariakoo jijini Dar
Apokonywa medali Olimpiki ya Pyeongchang