Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemwagia sifa Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita kwa kuwa na msimamo wa kuto yumbishwa na msimamo wa vyama vya siasa.

Meya Mwita ambaye ni Diwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alikuwa ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya maji yanayoendelea nchini.

Makonda ametoa sifa hizo mara baada ya Mwita kuzungumza na kumkaribisha mkuu huyo wa mkoa kutoa hotuba yake kwa wananchi.

“Meya nilijua utazungumzia maandamano, ila niseme wazi namkubali sana Mwita, ni miongoni mwa watu ambao unaweza ukakaa nao kuzungumzia suala la maendeleo,”amesema Makonda

Amesema kuwa Meya Mwita hana tabia kama za wenzake ambao ni wapinzani na muda mwingi huwa anawaza kuwaletea maendeleo wananchi.

Hata hivyo, Makonda amezungumzia maandamano yanayohamasishwa mitandaoni, kwa kusema kuwa kuna watu ambao wanatamani kuiingiza nchi katika machafuko.

Video: Lissu amvaa JPM, Vigogo watano TPDC kizimbani
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 17, 2018