Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemtaka Meya wa Ubungo, Boniphas Jacob kuwa na nidhamu kwa kutambua michango ya serikali inayotolewa katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Ameyasema hayo jijiini Dar es salaam wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo aliyoifanya katika jimbo la Ubungo, ambapo Meya huyo alieleza kuwa yeye ndiye aliyeweza kupeleka miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.

Aidha, baada ya kupata maelezo ya miradi mbalimbali ya maendeleo kutoka kwa Meya huyo, Makonda alimtaka Boniphas Jacob kuwa na heshima na shukrani kwa serikali ambayo inampatia fedha za kuendeshea miradi hiyo na siyo kujisifia.

“Meya wa Ubungo amekosa nidhamu kwa kudanganya wananchi kuwa yeye ndio amefanikisha mradi wa ujenzi wa Kisima cha Maji Kata ya Mbezi Makabe wakati Rais Dkt. John Magufuli ndio aliyetoa fedha hizo kiasi cha Shilingi Milioni 611,”amesema Makonda

 

Video: Ukikutwa na mfuko mmoja wa plastiki faini sh30,000, CAG Assad aivuruga CCM
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Aprili 25, 2019

Comments

comments