Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemuagiza msanii wa muziki wa bongo fleva, Amber Rutty kufika kituo chochote cha Polisi kabla ya saa 12 Jioni.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii, Makonda amechapisha picha ya mwanadada huyo na kuandika ujumbe wa kumtaka ajisalimishe kituo chochote cha polisi.

“Wakati TCRA wakijipanga kuchukua hatua, mimi namtaka mwenye picha hii kufika kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu na eneo lake kabla ya saa 12 jioni. na ukifika waambie umeitwa na RC Makonda watakupatia ujumbe wako,”ameandika Makonda

Aidha, video ya mwanadada huyo yenye maudhui ya kingono, imesambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua taharuki kubwa kwa jamii na vyombo vinavyohusika na kusimamia wasanii ikiwemo BASATA.

Hata hivyo, tayari msanii, Amber Rutty amejitokeza na kuomba radhi kutokana na kusambaa kwa video hiyo, huku akishindwa kufafanua mazingira ya kurekodiwa na hata kusambaa kwake.

Romania kucheza bila mashabiki
TPA yawataka Wahandisi kuchangamkia fursa

Comments

comments