Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amenasa rundo la mifuko ya sukari lililokuwa limehifadhiwa katika ghorofa linalojengwa wilaya ya Kinondoni jijini humo.

Mtanzania mwenye asili ya bara la Asia, ambaye alikiri kuwa mmiliki wa mifuko hiyo ya sukari inayokadiriwa kuwa takribani tani kadhaa alimueleza Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa yeye hukusanya mifuko hiyo ya sukari na kuigawa bure kwa wafanyakazi wake pamoja na wananchi.

Alisema kuwa sukari hiyo imeingia katika jengo hilo miezi sita iliyopita na kwamba hajawahi kufanya biashara ya sukari.

“Hata hawa wafanyakazi walioko hapa ukiwauliza, hii sukari imeingia hapa zaidi ya miezi sita iliyopita na huwa nawagawia,” alisema mmiliki huyo.

Hata hivyo, Makonda aliwataka Polisi waendelee kumhoji huku akimueleza kuwa hata utoaji wa misaada una taratibu zake.

“Kila kitu unachokifanya kina utaratibu wake. Kama unagawa sukari kuna utaratibu wa kugawa na ukiuza pia kuna utaratibu wa kuuza. Hapa tulipo tuko kwenye operesheni na ndio maana nimeacha watu wanakagua jengo lote. Na taarifa tulizonazo ni kwamba mna utaratibu wa kupeana hizi sukari ili kutoa kule mlikoficha,” alisema Makonda.

Hata hivyo, mmiliki huyo alisisitiza kuwa hajaficha sukari hiyo na anaimiliki kwa lengo la kuigawa tu.

Mtu huyo aliendelea kuhojiwa na polisi baada ya Mkuu wa Mkoa aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Akly Hapi kuondoka.

Magufuli aiweka kando safari ya London, amfuata Museveni
Video Mpya: Nay wa Mitego – Saka Hela