Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameomba radhi watu wote waliokerwa na kauli yake ikisema kuwa hakuwahi kutegemea wala kuona Mchaga angeweza kutoa msaada kwa walemavu na kwamba, ni jambo la kushangaza.

Makonda alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza wakati wa kuaga mwili wa Dk. Reginald, aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Akiwa kwenye madhabahu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Moshi mkoani Kilimanjaro, Makonda ameomba radhi na kumshukuru katibu wa CCM kwa kumuombea msamaha akisema kwamba, kitendo hicho kinaashiria upendo aliokuwa nao kwake.

“Baba Askofu na kaka yangu Mbowe na ndugu zetu, nashukuru sana kwa maelekezo na maonyo yenu, lakini pili nashukuru sana kwa katibu wangu mkuu kusimama na kuomba radhi kwa niaba yangu, huu ni upendo mkubwa sana,” amesema Makonda.

Aidha, Kauli hiyo ya Paul Makonda kwamba hakuwahi kutegemea kuona Mchaga angeweza kutoa msaada kwa walemavu na kwamba, ni jambo la kushangaza, imekera wengi.

Hata hivyo, Makonda amesema kuwa, kuna tafsiri mbaya pale aliposema kuwa, wachaga hawasaidii watu na kwamba, Dk. Mengi ndiye aliyemshuhudia.

Kwenye madhabahu hayo Askofu Shoo aliamua kumuita Mbowe na kupeana mkono na Makonda ikiwa ni ishara ya kuombana msamaha mara baada ya Mbowe kukemea vikali kauli za ubaguzi na kusema kuwa watu wote wanatakiwa kuzikemea kauli hizo kwani hazijengi nchi bali zinabomoa.

“Tusitengane kwa makabila yetu. Naomba wale wote walioguswa na kauli ile, nitoe msamaha kwa kumuaga Mzee Mengi,… anapotokea kiongozi mwenye mamlaka, wakatoa kauli za kibaguzi, lazima tuungane wote kupinga,” alisema Mbowe kwenye shughuli hiyo.

Dk. Bashiru amesema, alishawahi kumkanya Makonda na kwamba, hii ni mara ya pili, akiongeza “ameanza kubadilika.”

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 10, 2019
Mbowe akemea kauli za ubaguzi

Comments

comments