Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema itamchukulia hatua mwekezaji aliyetoa ardhi kwa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, kwa madai kuwa ardhi aliyoitoa siyo yake.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema mwekezaji huyo aliidanganya Serikali pamoja na kumdanganya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ambaye ndiye aliyekabidhiwa eneo hilo kwa niaba ya Serikali.

Mbali na kosa la kuidanganya Serikali, Lukuvi  amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara huyo kwa kumiliki ardhi kinyume cha sheria.

Aidha, Kuhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, Lukuvi amesema tayari amefanya  mawasiliano na kumuelewesha kuwa alidanganywa kwa kuambiwa kuwa anapewa eneo kwa ajili ya viwanda, huku eneo lenyewe likiwa ni mali ya Serikali.

Hata hivyo, mara baada ya makabidhiano hayo eneo la Kisarawe II Wilaya ya Kigamboni Mkurugenzi huyo alisema wameamua kumkabidhi eneo hilo ili kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuijenga Tanzania ya viwanda na kuwakomboa wananchi wenye uchumi wa kati.

Kwa upande wake Makonda alieleza kuwa dhamira ya viwanda ya Rais Magufuli inabidi itafsiriwe kwa vitendo, hivyo eneo hilo litatumika kwa ajili ya Ufugaji, Kilimo, Usindikaji, Utengenezaji wa sabuni na eneo hilo litatumika kwa Wilaya zote

Magazeti ya Tanzania leo Februari 28, 2017
Zitto Kabwe anena kuhusu Lema, ataka ofisi ya DPP iwajibishwe