Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda mapema leo hii amekabidhiwa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi Milioni 400 kutoka kiwanda cha MMI Steel LMT kwa ajili ya kampeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam.

Vifaa alivyokabidhiwa ni Mabati 15,000 yenye thamani ya shilingi Milioni 360, Nondo Tani 22 zenye thamani ya shilingi Milioni 40 ambapo pia kiwanda kimemuahidi kumpatia Rc Makonda vifaa vingine ikiwemo Rangi, Nondo na Mabati.

Rc Makonda amekishukuru kiwanda cha MMI Syeel LMT chini ya Mkurugenzi wake Subhash Patel kwa kuwa mdau mkubwa wa kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu na kuwasihi wadau na wananchi kujitokeza kuchangia kampeni hiyo ili kutoa heshima kwa walimu.

Aidha Rc Makonda amesema kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri ambapo hivi karibuni atapokea kontena nyingine 16 za Furniture kutoka Marekani kontena 10 za vifaa tiba kutoka Uingereza na kontena 10 za Maziwa kutoka China kwa ajili ya Watoto waliojitokeza wakati wa zoezi la kutafuta haki ya watoto waliotelekezwa kama sehemu ya msaada.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha MMI Steel LMT, Subhas Patel amesema wameamua kutoa vifaa hivyo kama sehemu ya kutambua umuhimu wa elimu na kuunga mkono jitihada za RC Makonda katika uboreshaji wa elimu kupitia mazingira bora ya walimu kufanya kazi.

 

West Ham yamnyemelea Manuel Pellegrini
Maaskofu 34 Chile wataka kujiuzulu