Wasanii wa jiji la Dar es Salaam hivi sasa wanapaswa kutoiweka kwenye orodha ya matembezi yao ‘nyumbani’ kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mkuu huyo wa Mkoa amewapiga marufuku wasanii wote ambao hawakuhudhuria katika uzinduzi wa kampeni ya Usafi ya jiji hilo, kufika nyumbani kwake.

“Lakini nashukuru wasanii wote ambao wamejuika nasi, na kwa kweli hichi ni kipimo cha kuwatambua marafiki zangu wa kweli ni wapi. Na mimi niwaambie tu, sitaki kuona msanii wowote nyumbani kwangu ambaye hawezi kuniunga mkono kwenye mambo yangu ya maendeleo,” alisema Makonda leo alipokuwa akizindua kampeni ya usafi katika viwanja vya Leaders Club jijini humo.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wasanii wachache ambao ni Mchizi Mox, Yamoto Band, Diamond na team ya Wasafi, Mwasiti, Queen Darleen, Salam TKM pamoja na Steve Nyerere wa bongo movies.

Idadi hiyo ilimkera Mkuu huyo wa Mkoa ambaye alitoa onyo pia kwa wasanii waliofika wakiwa wamechelewa.

“Sitaki hiyo tabia, nimemuona Steve Nyerere hapa amekuja akiwa amechelewa hilo ni onyo, ukirudia tena nakushughulikia. Huwezi kuwa rafiki yangu alafu kwenye mambo kama haya huangaiki, wengine wanataka waombwe, eti mbona hujanipigia simu kuniomba nipost, we nani?. Swala la usafi siyo la serikali ni swala kila mtu,” aliongeza Makonda anakaririwa.

Video: Davido aonekana akimpiga ‘shabiki’ kama mwizi
Uganda, Tanzania wapeana neema nyingine ya gesi