Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza oparesheni maalum dhidi ya magenge ya uhalifu mkoani humo ambayo inatarajia kuanza hivi karibuni.

Makonda ameweka wazi maandalizi ya oparesheni hiyo maalum muda mfupi kabla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa hostel za wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mapema leo. Ameyasema hayo wakati akitoa salaam za Rais John Magufuli atakayeweka jiwe la msingi katika mradi huo.

Amesema kuwa ofisi yake inaandaa oparesheni hiyo ya kuyafuta magenge hayo ya uhalifu kwakuwa ndio changamoto inayoukabili mkoa huo kwa sasa.

Tangu alipoteuliwa, Makonda ameshaendesha oparesheni mbalimbali na hivi karibuni alianzisha kampeni ya kupanda miti iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa.

 

Waziri Mkuu arejea Dar akitokea Arusha.
Ray C aingia ‘jikoni’ na Damian Soul