Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametangaza vita kwa wafanyabiashara wanaouza Sukari kwa bei ghali tofauti na bei elekezi ya Serikali ambapo amesema ifikapo Kesho kikosi kazi kitafanya ukaguzi na watakaobainika kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya juu Watakamatwa na Sukari kutaifishwa na Serikali.

RC Makonda amewaelekeza wakuu wa wilaya zote tano za Mkoa huo kuhakikisha msako huo unaanza kesho na asisalie mfanyabiashara yoyote anaeuza Sukari hiyo kwa bei ya juu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Makonda kubaini uwepo wa baadhi ya wafanyabiashara wanaouza Sukari kwa bei ya hadi Tsh 4,500 kinyume na bei elekezi ya serikali ya Tsh 2,600 jambo linalopelekea maumivu na gharama kwa wananchi.

Mapema wiki iliyopita waziri wa Viwanda na biashara, Innocent Bashungwa alitangaza bei elekezi ya sukari kwa mikoa yote hapa nchini ikiwemo Dar es salaam ambapo bei yake elekezi ni 2,600.

Ngoma za Diamond kuanza kupigwa Clouds, Yope remix yafungulia
Corona: Waziri aagiza Mkurugenzi Maabara ya Taifa asimamishwe kazi