Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda ametoa kiasi cha shililingi milioni kumi kwa Said kijana aliyetobolewa macho na Scorpion, hiyo ni kufuatia ahadi  aliyoitoa ya kumsaidia kijana huyo katika maisha yake.

Pamoja na msaada huo wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda kwa Kijana huyo ambao ameutoa kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds Tv, pia Staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz nae alikuwepo kwenye kipindi hicho ambapo amemkabidhi milioni mbili.

Pia, GSM imeahidi kumnunulia nyumba Said Ally, huku kampuni ya TSN wakitoa pikipiki mbili, pia Said amepata pikipiki tatu kutoka kwa wadau wengine na kufanya jumla ya pikipiki tano.

Kwa upande wake Said ametoa shukrani za dhati kwa wote walio pamoja naye kwa misaada mbali mbali huku shukrani nyingi akizielekeza kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. Bofya hapa kutazama video

Video: Makonda atimiza ahadi yake kwa kijana aliyetobolewa macho na Scorpion, kununuliwa nyumba, pikipiki 5 na bajaji 2
Video: Diamond atoa msaada wa sh. mil. 2 kwa kijana aliyetobolewa macho na Scorpion