Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemuagiza Diwani wa kata ya Ubungo ambaye ni Meya Mteule wa Manispaa hiyo, Boniphace Jacob kuhakikisha anamaliza changamoto ya madarasa matano katika shule  ya Sekondari Urafiki.

 Amesema hayo alipokuwa akizindua shule hiyo ya urafiki ikiwa ni moja ya muendelezo wa ziara ya siku 10 kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda amewataka viongozi wa kisiasa kuweka siasa pembeni na badala yake wawatumikie wananchi.

“Diwani wa hapa inabidi upambane na kuhakikisha uhaba wa vyumba hivyo vitano vya madarasa unakamilisha mapema zaidi ili wanafunzi wasome”alisema Makonda.

katika hatua nyingine, Makonda amewataka wanafunzi kujitahidi kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kuingia katika soko la ushindani wa ajira.

Katika ziara hiyo pia ametembelea barabara ya Ubungo River Side na kuwataka wananchi wajitolee maeneo yao ili kupisha ujenzi wa barabara ambao ulikuwa ni changamoto kwao.

Audio: Tetemesha yamtambulisha Coyo na ngoma kali ‘Njoo Baadae’
Pochettino: Chelsea Wana Bahati Ya Kipekee