Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amebariki rasmi ndoa inayotarajiwa kufungwa hivi karibuni na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa kituo cha Radio cha EFM, Majizo pamoja na msanii wa maigizo ya filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kama Lulu.

Leo kupitia kurasa wake wa instagram Makonda amesema yeye kama mwenyekiti wa kamati ya harusi hiyo ameupitisha wimbo wa Harmonize na Mrisho Mpoto uliachiwa hivi karibuni unaojulikana kama “Nimwage radhi” kuwa ni wimbo utakaotumika katika harusi yao.

“Nikiwa Mwenyekiti wa kamati ya harusi ya ndugu Majizo na Bibi Elizabeth Michael (Lulu) nimeupitisha huu wimbo wa Mrisho Mpoto na Harmonize kuwa ndio wimbo rasmi wa harusi yao” amesema Makonda.

Ameongezea kuwa tarehe ya hurusi itatolewa na chaneli mpya radio ya EFM iliyoanzishwa jijini Dodoma.

Aidha Elizabeth Michael mnamo Mei 12 mwaka huu alipata msamaha wa rais kufuatia kifungo kilichokuwa kinamkabili kufuatia kesi yake ya mauaji bila kukusudia ya msanii mwenzake Steven Kanumba.

 

Magazeti ya Tanzania leo Mei 31, 2018
Zitto, Mbowe waungana kulichukua jimbo la Bilago

Comments

comments