Operesheni tumbua majipu bado inaendelea, ambapo jana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alimtumbua Mhandisi wa Mkoa, Josephat Shehemba.

Makonda alitangaza kumsimamisha kazi Mhandisi huyo  kwa kile alichoeleza kuwa ameshindwa kusimamia ipasavyo ujenzi wa barabara mkoani humo hali inayopelekea ujenzi wa barabara chini ya kiwango.

Alisema kuwa Mhandisi huyo ameshindwa kufanya kazi yake ipasavyo na kusababisha wakuu wa Wilaya na watendaji wengine kufanya kazi hiyo, huku yeye akiwa mstari wa mbele kudai malipo ya makandarasi waliojenga barabara hizo.

“Ameshindwa kusimamia lakini anakuwa mtu wa kwanza kudai fedha za kuwalipa wakandarasi ambao wamejenga barabara chini ya viwango angepaswa kusimamia atakapokwama au kumuona mkandarasi ameshindwa kufanya kazi yake kwa viwango basi angenieleza ili tuone tunafanya utaratibu gani,” alisema.

Mkuu huyo wa Mkoa alieleza kuwa hatamvumilia mtendaji yeyote ambaye atashindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo.

Katibu Mkuu Mpya Wa Simba Atema Cheche
Wananchi watinga Mahakamani Kudai ‘Bunge Live’