Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo amekabidhi kadi 220 za Bima ya Afya (Toto Afya Card) zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 11 kwa watoto yatima waishio kwenye mazingira magumu ili wapate uhakika wa matibabu ya mwaka mzima ikiwa ni sehemu ya mwezi mtukufu.

Makonda amesema kwa kawaida mwezi wa Ramadhan watu wamekuwa wakifuturisha watoto yatima lakini inakuwa ni chakula cha siku moja hivyo katika mwendelezo wa mwezi mtukufu ameona ni vyema aguse maisha ya watoto yatima kwa kuwapatia uhakika wa matibabu kwa kuwapatia Bima ya Afya ambapo ameamua kuanza na watoto 220 na baadae kuongeza wengine.

Aidha RC Makonda amesema kadi hizo zitawawezesha watoto kupatiwa matibabu bure kwa kipindi cha mwaka mmoja katika hospitali yoyote hapa nchini.

Pia ameongezea kuwa watoto waliopatiwa kadi hizo siku hii ya leo hawahusiani na wale waliojitokeza kwenye zoezi la kutafuta haki ya mtoto ambapo ameshukuru Hospitali ya Regency na TMJ kujitolea kutoa kadi hizo.

Sambamba na hilo Makonda amesema atakabidhi mabegi 400 yaliyosheheni vifaa vyote vya shule kwa vituo vya watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu ili wawe na uhakika wa kupata masomo mwaka mzima na kuweza kutumia vyema fursa ya elimu bure.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Hospital ya Regency Dr.Kanabar Rajni na Mkurugenzi wa Hospitali ya TMJ Bi. Parul Chhaya kwa pamoja wamesema wameguswa kutoa msaada huo kama sehemu ya kuunga mkono hamasa anayoitoa RC Makonda kwa wazazi kuwa na kadi za bima za afya (Toto Afya Card).

Video: Rais Magufuli amjaza noti aliyelalamikia barabara Kinondoni
Kilimo cha umwagiliaji kutatua changamoto za mabadiliko ya Tabianchi

Comments

comments