Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemtaka Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kutangaza baadhi ya mambo ambayo yamefanywa na Rais Magufuli kufuatia ziara yake katika baadhi ya nchi Ulaya.

Makonda ameandika kuwa shukrani kwake muumba wa mbingu na ardhi kwa kumpa kaka yetu Tundu Lissu afya na siha njema.

“Wengi walioko jimboni Singida na Watanzania wote walihangaika kwa sala na maombi, usiku na mchana, wengine wakichanga pesa zao na hatimaye mola akajibu maombi yao.” ameandika Makonda.

Aidha, ameongeza kuwa kwa heshima na kuonyesha uzalendo, amemshauri Tundu Lissu kurudi nyumbani ili aweze kutoa shukrani kwa watu wake kwani wamemmiss zaidi ya hao anaowakimbilia kwasasa.

Hata hivyo, Makonda amesema kuwa ziara ya Lissu barani Ulaya haina tija kwa yoyote zaidi ya kuichafua Serikali na si kumchafua  Rais ni kuichafua Tanzania yote.

Nandy afanya ngoma mpya na Mr.Blue, Tazama
Kamati ya Maendeleo ya Kata yamgomea DC

Comments

comments