Mkuu wa Mkoa wa Dar es salama Paul Makonsada amewataka wazazi na walezi kuwapa uhuru watoto kuchagua masomo wayapendayo, na kuongeza kuwa Tanzania inauhaba wa wataalamu katika idara mbalimbali hivyo kuwachagulia masomo watoto ni kuwaongezea mzigo usiowafaa.
Amesema hayo aliopokuwa katika mahafali ya kidato cha Nne ya shule ya Sekondari ya Jitegemee iliyopo jijini Dar es salaam, Makonda amesema Tanzania ina kila aina ya utajili na watu wengi wanaofanya kazi katika maeneo mbalimbali ambayo ni muhimu ni watu kutoka nje ya nchi.
Aidha, Makonda ametoa ahadi ya kuwasomesha wanafunzi wa kuanzia wa kwanza hadi wa tatu watakaofaulu vizuri katika masomo ya sayansi kwa Mkoa wa Dar es salaam, atawapeleka shule yeyote watayotaka kwenda kusoma hapa nchini, ameongeza kuwa Tanzania haina tatizo la ajira bali ni kukosekana kwa ubunifu kwa watanzania wengi ambao wamekuwa wakitegemea ajira
Katika hatua nyingine Makonda amewaasa wanafunzi hao kutobweteka na kutegemea ajira bali wajijengee fikra za kujiajili na si kuajiriwa kama ilivyo kwa sasa, ”Wanafunzi mnaomaliza kidato cha Nne jengeni fikra za kuajiri watu kwa sasa ili mkimaliza vyuo moja kwa moja mkaanzishe shughuli zenu wenyewe”.alisema Makonda.