Baba Mlezi wa WCB ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa pongezi za dhati kwa mshindi wa tuzo za BET, 2017 RayVanny pamoja na uongozi wake kwa kazi nzuri wanayoifanya kuipeperusha vyema bendera ya taifa ya Tanzania.

Kufuatiwa pongezi hizo baba mlezi wa lebo hiyo, Paul Makonda amewakaribisha WCB katika chakula cha jioni leo nyumbani kwake baada ya uzinduzi wa karanga kariakoo.

Jana Rayvan amewasili  nchini Tanzania na tuzo hiyo aliyojishindia katika kipengele cha Viewers Choices Best New International Act, na kuwalaza wasanii wengine kutoka mataifa mengine kama Afrika Kusini, Korea Kusini na Jamaica.

Hivyo kupitia ukarasa  wa Instagram wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ametuma salamu za pongezi kwa Rayvany na Uongozi wake.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam katika ukurasa wake wa Instagram ameandika

”Mnaendelea kutupa heshima vijana huku mkipeperusha bendera ya taifa lenu, kwa ujasiri mkubwa naona fahari kuwa mlezi wenu. Mama yenu kawaandalia dinner saa moja tukutane nyumbani  baada ya kuzindua karanga zetu leo jioni kariakoo, huku mkijiandaa na kesho kuwasha moto nchini CONGO bila kusahau Rwanda inawangoja . Duh ratiba imebana”.

 

 

 

 

 

Bafetimbi Gomis Atimkia Uturuki
R.Kelly atambua uwepo wa Davido, afanya nae Remix