Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametimiza ahadi ya kusaidia gharama za matibabu ya mshindi wa BSS 2009 Pascal Cassian kwa kumkabidhi tiketi ya ndege, pesa ya nauli, chakula, hotel na pesa ya kujikimu kwa watu watatu watakaomsindikiza akiwemo mke wake na Mkuu wa kitengo cha Urolojia Hospital ya Taifa Muhimbili.

RC Makonda amesema uamuzi wa kumpeleka Nchini India ni baada ya Jopo la madaktari bingwa wa Muhimbili kuridhia na kumtafutia Hospitali ya kimataifa nchini India yenye uwezo wa kutibu tatizo hilo.

Aidha, RC Makonda amewashukuru watanzania wote waliochangia na kufanikisha safari hiyo na kuwaomba wazidi kuwa na moyo huo huo wa kusaidia kwenye matatizo.

Kwa upande wake Pascal Cassian amemshukuru RC Makonda kwa kuona maumivu aliyokuwa akiyapata na kuamua kumsaidia ambapo ameeleza kuwa anaamini atarejea nchini akiwa amepona kwa uweza wa Mungu.

Itakumbukwa RC Makonda aliamua kumsaidi Pascal kwa kumtoa nyumbani na kumpeleka hospitali baada ya kuona kupitia Dar24 Media.

Pascal alipata ajali iliyopelekea tatizo kubwa kwenye mfumo wake wa figo.

Wimbo wa Vanessa watumika ligi ya kikapu Marekani
Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine

Comments

comments