Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeruhusu kufunguliwa kwa kesi ya jinai dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Ruhusa hiyo ni majibu kwa Saed Kubenea ambae aliwasilisha maombi katika mahakama hiyo baada ya mahakama za Hakimu Mkazi za Kisutu na Kinondoni kukataa kufungua mashitaka dhidi ya kiongozi huyo.

Barua ya Saed Kubenea akimshtaki Paul Makonda

Katika barua hiyo, Naibu msajili wa Mahakama kuu, Joseph Luambano ameeleza kuwa Kubenea anayo haki ya kufungua kesi ya Jinai dhidi ya Makonda.

Kubenea ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, anamshutumu Paul Makonda kwa makosa tofauti ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na kuvamia kituo cha Televisheni cha Clouds Media Group na kuingilia urushaji wa matangazo ya kipindi Machi 17, 2020.

Hapo awali ombi la kufungua kesi hiyo lilikataliwa na mahakama za Hakimu Mkazi Kisutu na Kinondoni kwa madai kuwa ni lazima kuwepo na hati ya mashitaka ya mahakama ya mwanzo.

Pia mahakama hizo zikaendelea kusema hapakua na kiapo cha kuonesha namna gani DPP ameshindwa kuchukua hatua za kumshtaki Makonda.

Katika Shauri la Kubenea, pia anawashitaki Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI na Mkurugenzi wa Mashitaka DPP ambao anadai walishindwa kumchukulia hatua za kisheria Makonda alipotenda makosa hayo.

Rais Samia ateta na mawaziri
Hofu yatanda, Miili yaendelea kuopolewa mtoni