Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesimamisha shughuli zote za mabaraza ya kata mkoani humo pamoja na kesi zote hadi hapo utaratibu wa kupitia upya taaluma za wanasheria waliopo katika mabaraza hayo utakapofanyika.

Makonda ameeleza kuwa wengi hawawezi kazi ndio maana wanashindwa kutatua migogoro ya ardhi na kusababisha Serikali kulaumiwa na wananchi.

Makonda ametoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee katika mkutano wa kupokea taarifa za malalamiko ya wananchi yaliyowasilishwa kwa wanasheria wa mkoa huo.

Makonda amewataka makatibu wa tarafa wote kuanzia Februari 12, mwaka huu kuanza kutembelea mabaraza hayo.

Pia amewataka wakurugenzi kupitia wasifu wa wakuu wa idara na kazi zote wanazofanya na kuamuru wakuu wa idara ya ardhi katika  manispaa ya Ubungo na Ilala kupangiwa kazi nyingine.

Amesema wanapaswa kusimamishwa kwa sababu migogoro katika maeneo yao ni mengi kuliko wanayoyataja, jambo ambalo linaonyesha kuwa hawako makini na kazi yao.

Pia ameeleza kuwa watu hawana imani na mahakama ndio maana wanapeleka kesi na malalamiko yao kwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, na wakurugenzi.

 

Young Afrcans waanza kwa ushindi kiduchu
Video: Makonda awatumbua wakuu wa Idara za Ardhi