Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa atavunja  nyumba zinazotumika kufanya biashara ya ngono, Maarufu kama uwanja wa fisi zilizopo Manzese jijini Dar es salaam na kujenga viwanda vidogo vidogo ambavyo vitawasaidia wananchi.

Ameyasema hayo alipokuwa katika muendelezo wa ziara yake ya kutembelea Jiji la Dar es salaam ikiwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuangalia namna ya kuzitafutia ufumbuzi, Makonda amesema kuwa nyumba zote zilizopo uwanja wa fisi zitabomolewa ingawa watu wanaoishi maeneo hayo wanaishi maisha magumu.

“Ili kuokoa sehemu ya madanguro tutabomoa na kujenga viwanda vidogo vidogo kama azima ya kuendeleza Serikali ya viwanda ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli”alisema Makonda.

Aidha katika hatua nyingine, Makonda alisema serikali itakamilisha ujenzi wa barabara inayoanzia kisiwani hadi Mwananyamala yenye kilometa 0.8 katika kiwango cha lami kulingana na umuhimu wake.

Bodi ya mikopo yadaiwa bilioni 1.7
Video: 'Lipumba ni msaliti' - Maalim Seif