Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa atawakamata watu wote wanaozurura katika jiji hilo bila kuwa na kazi.

Akizungumza jana na waandishi wa habari akiwa ameambatana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii.

“Kuanzia Jumatatu, Aprili 4, 2020 tutakamata wazururaji wote wanaozurura mjini bila kuwa na kazi ya maana. Hao ndio wanaosababisha mikusanyiko isiyokuwa na tija,” amesema Makonda.

“Unaenda stendi huna kazi, unaenda sokoni na huna kazi, unaenda bandarini, feri na huna kazi huo ni uzururaji. Na sio tu kwamba una hatarisha maisha yako una hatarisha na maisha ya wengine ambao umewaacha majumbani,” aliongeza.

Serikali imeendelea kuhamasisha wananchi kujikinga na virusi vya corona ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni.

Hadi sasa, kumeripotiwa visa 22 nchini Tanzania.

Chui-milia akutwa na virusi vya corona
Corona: Masanja asimulia alivyohojiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Dodoma