Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameunda kamati ya watu 18 kutoka makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo wanaharakati na wanasheria wa kutetea haki za watoto na wanawake kwa ajili ya kutatua tatizo la ongezeko la watoto wa mitaani.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam, ambapo ameipa kamati hiyo mwezi mmoja ili kuja na njia zinazopaswa kutumika kudhibiti tatizo hilo ambapo amesema, utafiti uliofanywa na Idara ya Ustawi wa Jamii, umeonyesha kuwa jiji la Dar es salaam pekee lina watoto waishio katika mazingira magumu elfu 5.

Hata hivyo, kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo na Wakili wa kujitegemea, Albert Msando amesema kamati yake itajielekeza katika kuangalia sheria na mapungufu yake kwa ajili ya kuzifanyia maboresho.

 

Mtoto wa Rais kumuoa ‘binti’ wa kiongozi wa upinzani
Ajali ya ndege yaua zaidi ya 100, watatu wanusurika