Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo Agosti 3, 2020 amekabidhi ofisi kwa Mkuu wa Mkoa huo wa sasa Aboubakar Kunenge, ambapo amesema amehitimisha safari yake ya ukuu wa mkoa.

Aidha Makonda amesema Rais Magufuli alimuamini na kuamini anachokifanya ndio maana aliibuka kidedea kudhibiti madawa ya kulevya katika mkoa huo.

“Rais aliniamini na kuamini ninachofanya ni kwa faida ya Watanzania na tukaibuka kidedea dhidi ya mapambano ya Dawa za Kulevya, JPM ni Rais msikivu kwangu tena mnyenyekevu na Mcha Mungu ambaye daima nitaendelea kumuenzi kwa vitendo”amesema Makonda

“Rais Magufuli aliamini katika Vijana nikiwa Kijana wa kwanza kupewa majukumu katika Mkoa mkubwa na kuacha alama itakayodumu milele, namshukuru JPM kwa mambo mengi ikiwemo uvumilivu wake, ukiteuliwa unaanza kufanya kazi, kazi unayofanya inaweza kuleta kelele na mbwa mwitu wengi wakawa wanabweka lakini Rais wetu aliziba masikio akaendela kuniamini na Tarehe 15 nimeondoka mwenyewe ikiwa ni ishara ya kukubali kazi niliyofanya na kuamini ya kwamba sasa umefika wakati uende kwenye majukumu mengine” amesema Makonda

Morrison na wenzake kutemwa Young Africans
Ajira: Nafasi za kazi kwa watangazaji, waandishi wa habari