Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amebainisha kuwa baba yake ni moja kati askari kutoka Tanzania ambao wamepigana vita nyingi kwa ajili ya kutetea taifa ikiwemo vita ya Kagera mwaka 1978.

Makonda amesema hayo wakati alipokuwa anatoa salamu kwa Rais Magufuli katika sherehe za ufunguzi wa kituo cha uwekezaji cha SUMA JKT Mgulani Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa alizaliwa na kulelewa katika kambi za jeshi

“Nikunong’oneze mheshimiwa Rais, mimi nimezaliwa kambini na baba yangu ni miongoni mwa askari waliopigana vita nyingi ikiwemo vita ya Uganda na mpaka ulemavu wake wa mguu ni kutokana na kazi ya kuipigania Tanzania,” amesema Makonda

Aidha, Makonda ameongeza kuwa kutokana na kulelewa katika kambi za jeshi imemsaidia kupata ujasiri wa kuongoza mkoa wa Dar es salaam wenye changamoto nyingi na kuweza kufanya kuwa Jiji la raha Tanzania.

Hata hivyo, katika tukio hilo, Rais Dkt Magufuli alizindua kituo cha uwekezaji cha SUMA-JKT ambacho ndani yake kuna kiwanda cha Ushonaji, Maji, Chuo cha Ufundi Stadi na Ukumbi wa Mikutano.

Sugu anena alivyowashtua wafungwa, heshima aliyopewa na askari gerezani
Kim Kardashian aonja ‘joto ya jiwe’ kwa kuweka tangazo la msosi