Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Malawi, Jane Ansah ametangaza tarahe ya uchaguzi wa marudio nchini humo kuwa ni Julai 2 mwaka huu.

Amesema uchaguzi huo wa marudio unafanyika baada ya Mahakama ya kikatiba nchini humo kutengua matokeo ya awali ambayo yalimpa ushindi Rais, Peter Mutharika.

“Kufuatia maamuzi ya Mahakama ya katiba ya Februari 3 yaliyofuta matokeo ya uchaguzi wa urais na kuagiza kufanyika uchaguzi mpaya kwasababu ya dosari natangaza uchaguzi mpya utafanyika Julai 2” Amesema Ansah.

Ikumbukwe kuwa Mei 21, 2019 Mahakama hiyo ilitangaza kutengua matokeo ya uchaguzi kwa hoja ya kuwa matokeo hayo yaligubikwa na udanganyifu mkubwa.

Licha ya rais Mutharika kukata rufaa na kusema uchaguzi kufanyika kwa mara ya pili ni gharama kubwa hivyo hauna haja, Mahakama ilitupilia mbali rufaa hiyo na kuagiza uchaguzi urudiwe ndani ya siku 150.

 

CORONA: Jiji la Kinshasa lafungwa, Rais atangaza hali ya dharura
Aliyekuwa mwenyekiti CCM Dodoma mkononi mwa Takukuru