Timu za vijana za Ghana na Mali zimefanikiwa kutinga fainali katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17 yanayofanyika nchini Gabon huku yakishuhudiwa na mataifa mbalimbali.

Aidha, Ghana wametinga fainali baada ya kupata ushindi wa penati 6-5 dhidi ya Niger baada ya kwenda sare katika dakika tisini za mchezo huo ambapo timu zote mbili zilionekana kutoshana nguvu.

Kwa upande wa mabingwa watetezi timu ya Mali wao wamefanikiwa kutinga fainali ya pili mfululizo baada ya kuiondoa Guinea kwa penati 2-0 huku kipa wa Mali Youssouf Koita, akiwa shujaa wa timu hiyo kwa kuokoa michomo mingi na penati

Mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya vijana utachezwa jumapili ya tarehe 28 katika dimba la Amitié Sino-Gabonaise, mjini Libreville, huku mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Niger na Guinea utafanyika siku hiyohiyo ya jumapili.

Video: Nani kumrithi Profesa Muhongo?, Tumeibiwa sana
Magazeti ya Tanzania leo Mei 25, 2017