Jeshi nchini Mali, limepokea ndege za kijeshi aina ya jeti za L-39 na Sukhoi-25, helikopta za Mi-24P na helikopta ya kivita kutoka nchini Urusi ambapo zilitambulishwa rasmi wakati wa sherehe maalum jijini Bamako.

Waziri wa Ulinzi wa Mali, Sadio Camara ametoa pongezi kwa kile alichokiita “ushirikiano wa ushindi na Shirikisho la Urusi” na Mali na kuongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuimarisha uwezo mpya wa upelelezi na mashambulizi.

Hakuna taarifa iliyotolewa, kuhusu masharti ya kupata msaada huo wa zana za kijeshi ingawa hapo awali silaha za Urusi zilizowasilishwa kwa mwaka huu, zilikuwa helikopta, rada za uchunguzi pamoja na mifumo ya rununu ya rada.

Mali, imekuwa ikikabiliwa na kampeni ya kijihadi iliyoanza kaskazini mwa nchi hiyo mwaka 2012 na kuenea hadi kusini mwa nchi hiyo ikiongozwa na waasi hadi kufika nchi za Burkina Faso na Niger.

Mapema hivi karibuni, magaidi wa Al-Qaeda waliongeza shinikizo kwa wanajeshi wa Mali, huku Mwezi Julai waasi wa jihadi wakishambulia kambi ya kijeshi ya Kati ya Mali nje kidogo ya mji mkuu wa Bamako ambako rais wa mamlaka ya mpito anaishi.

Ngilu ailalamikia IEBC kwa kuchapisha jina lake
Juma Kaseja, KMC njia panda