Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) imesema kuna mabadiliko ya mfumuko wa bei ndani ya miezi miwili kutokanana na kupanda kwa baadhi ya bei za bidhaa ikiwemo malimao na vitunguu swaumu ambazo zinatumika kujifukiza kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

Hayo yamebainishwa na kaimu Mgurugenzi wa sensa ya watu na Takwimu za jamii Ruthi Minja akizungumza na waandishi wa habari, amesema fahirisi ya bei zimeongezeka asilimia 0.4 kutokana na uhitaji mkubwa wa bidhaa hizo kuongezeka ikilinganishwa na miezi miwili iliyopita.

Amesema kuwa mfumuko wa bei kwa mwezi april 2020 umepungua hadi asilimia 3.3 kutoka asilimia 3.4 kwa mwaka.

”Kama mnavyofahamu hivi sasa malimao na vitunguu swaumu vinatumika sana inawezekana mahitaji yameongezeka zaidi na kuchangia kongezeka kwa bei kuliko ilivyo awali kwa kipindi cha mwezi mmoja huu” amesema Ruth.

Amesema kuwa bei zimeongezeka hadi 120.67 kutoka120.20 mwezi machi 2020 kuongezeka kwa bei kumechangiwa na kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa ya vyakula na visivyo vyakula ambapo samaki wamepanda kwa asilimia 1.4 ,malimao 5.7 , vitunguu swaumu 3.4, njegere 4.0, na viazi asilimia 5.9.

Parimatch yaja kibabe na mfumo mpya
Uganda: Madereva wazidi kuongeza visa vya Corona, Museveni atangaza maombi