Rais Shirikisho la soka nchini  (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Alexander Ceferin kuchaguliwa kuwa Rais Mpya wa Shirikisho la soka  barani Ulaya (UEFA) katika uchaguzi mkuu uliofanyika jijini Athens nchini Ugiriki Jumatano Septemba 14, 2014.

Katika salamu zake, Rais Malinzi ameelezea kuwa kuchaguliwa kwa Ceferin  ambaye ni Rais wa Chama cha Soka Slovakia ni kilelelezo cha familia ya mpira wa miguu ya Ulaya kuona umuhimu wake katika kutumikia shirikishi hilo sambamba na kuwa kiongozi wa FA ya Slovekia.

Rais Malinzi amesema ana imani na Ceferin kuwa ataweza kutumikia vema nafasi zote. Malinzi ana imani Caferin ataunganisha nguvu kwa maendeleo ya soka kwa kushirikiana na Rais wa Shirikisho la soka duniani (FIFA), Gianni Infantino na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou.

Ceferin amechaguliwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Michel Platini ambaye alifungiwa na FIFA kwa miaka minane Baada ya kukutwa na kosa la kupokea rushwa ya Pauni 1.3mil.

Rais huyu mpya alimshinda Michael Van Praag Rais wa chama cha mpira cha Uholanzi katika kura zilizopigwa huko Athens. Ceferin atashika kiti hicho cha uraisi mpaka mwaka 2019.

Wenyeji CECAFA Challenge Kupambana Na Kilimanjaro Queens
Mshike Mshike Wa Ligi Kuu Bara Kuendelea Tena Kesho