Rais wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Jamal Malinzi amekanusha uvumi wa kuhusika katika tuhuma za upangaji matoke ya michezo ya mwisho ya ligi Daraja la kwanza.
Malinzi amekanusha uvumi huo baada ya ya taarifa za awali kudai kwamba TFF kupitia kwa kiongozi huyo walihusika katika upangaji wa matoke ya mechi za mwisho aa ligi Daraja la kwanza mapema mwezi huu.
Malinzi amesema kwa yeyote mwenye ushahidi ambao utaonyesha anahusika na hatua ya upangaji wa matokeo apelike katika vyombo husika vinavyohusu masula ya utoaji na upokeaji wa rushwa (TAKUKURU).
Hivi karibuni kulikuwa na na taarifa kuwa Malinzi alikuwa akiwasiliana na baadhi ya viongozi wa michezo hiyo ili waweze kufanikisha timu za kanda ya ziwa kucheza ligi kuu katika msimu ujao wa ligi hiyo.