Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Annamaria Jose Raphael Gonzalez ambaye ameambukizwa Virusi vya Corona ameripotiwa kujifungua watoto mapacha katika Hospital General La Villa, huko Mexico City.

Gonzalez mwenye umri wa 34, amejifungua watoto hao ambao wameaonekana kuwa wenye Afya majira ya saa 2 asubuhi na kumpa jina la Corona mtoto wake wa kike huku wakiume akimpa jina la Virus.

Watoto hao wawili amewaita Corona Jose Miguel Gonzalez na wakiume Virusi Jose Miguel Gonzalez baada ya kupata ushauri wa majina hayo kutoka kwa Daktari.

”Sikupanga jina la kuwaita hapo kabla , daktari mmoja alipendekeza niwaite Corona na Virus kwa sababu nilikuwa nimeambukizwa Covid 19 niliona ni wazo zuri” Gonzalez alimwambia mwandishi wa habari.

Kwa upande wake Daktari, Eduardo Castillas wa Mexico Hospital General La Villa amesema kuwa alikusudia majina hayo kama utani. Hata hivyo dokta huyo ameongeza kuwa habari njema ni kuwa mama huyo na wanawe wote wanaendelea vizuri.

“Nilimwambia kama utani anapaswa kuwaita Corona na Virusi lakini inaonekana aliipokea kwa uzito,” Daktari Eduardo Castillas alisema huku akicheka.

Annamaria Gonzalez alikusudia kujifungulia nchini Marekani lakini alishindwa kufikia malengo hayo hatakabla ya kuvuka boda.

“Nilijua nimeambukizwa virusi vya corona, lakini nilihitaji wanangu nijifungulie Marekani ili waweze kupata uraia wa nchi hiyo kwa kuvuka boda.” Ameeleza mama huyo

Video: Lissu,Spika Ndugai mnyukano mpya, Shahidi aeleza mazito kesi ya Zitto
Kampuni 10 zatangaza nafasi za ajira hapa

Comments

comments