Mwanamke mmoja katika kijiji cha Nyahera Kaunti ya Kisumu nchini Kenya, amewakatakata mapanga mpaka kifo watoto watatu wa mke mwenzie na kisha mwenyewe kujinyonga.

Tukio hilo limeelezwa kwamba mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la Jacinta Otieno, aliwaita watoto hao wanne kwenda kunywa uji nyumbani kwake.

Ndipo alipoanza kuwacharanga na mapanga mpaka kuwaua na yeye  mwenyewe kujinyonga, huku mtoto mmoja akinusurika baada ya kukataa kwenda kunywa uji.

Jacinta alifanya tukio hilo baada ya mke mwenza kwenda kanisani na kuwaacha watoto peke yao nyumbani ambako wanaishi jirani, huku mume wao akiishi jijini Nairobi na watoto wake wengine.

Kwa mujibu wa majirani, wawili hao wameelezwa kuwa hawakuwa na maelewano mazuri kutokana na wivu kwa mume wao, na kwamba Jacinta alishajaribu kutaka kujiua wiki moja iliyopita.

Watoto hao waliouawa walikuwa na umri wa miaka 7, 4 na 2, walikuwa wa mke mwenzie Hellen Otieno.

Hizi chokochoko za wapinzani tunazimudu- Kingu
Naibu Katibu Mkuu Bavicha ajiuzulu