Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kumkamata mwanamke Janeth Peter (32), mkazi wa Kiwira wilayani Rungwe kwa tuhuma za kumtupa mtoto wake mwenye umri wa siku tatu ndani ya shimo la choo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo Ulrich Matei, amesema,  mtuhumiwa huyo amekamatwa Oktoba 20, 2021 majira ya saa 1:00 usiku baada ya Polisi kufanya msako mkali katika Kata ya Kiwira na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye amehojiwa na kukiri kutenda kosa hilo.

Kamanda Matei amesema hadi sasa wanaendelea  kumhoji  pamoja na uchunguzi wa kitabibu kwa kushirikiana na wataalam wa afya ili kufahamu endapo alitoa mimba au ana matatizo ya kiafya sambamba na kufahamu sababu ya kufanya tukio hilo la kinyama.

Nilivyolazimisha Nyota na Kuambulia maumivu
Fursa za uwekezaji Tanzania zaendelea kukua