Huko nchini Nigeria mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Abuchi Odo (40), mwendesha bodaboda maarufu kama Keke ametaka kuikimbia familia yake mara baada ya mke wake, Ndindi kujaaliwa kujifungua watoto mapacha watano akieleza kuwa hana uwezo wa kuwalea watoto hao.

Jamaa huyo ameshangazwa na baraka aliyopata huku akilalamika kuwa hana uwezo wa kuwalea watoto hao watano.

Mkewe mwenye umri wa miaka 30 alijifungua watoto wanne wa kiume na mmoja wa kike kwa upasuaji katika zahanati Mercy Maternity, jimbo la Anambra nchini Nigeria.

Jarida la TUKO.co.ke limebainisha kuwa hii ni mara ya pili familia hiyo kubarikiwa mapacha hapo awali, mama huyo alijifungua mapacha watatu.

Abuchi Odo (40) amefunguka na kueleza kuwa alishtuka alipopata habari kuwa mkewe alijifungua watoto watano na hata akataka kutoroka akihofia jinsi atakavyowalea.

”Mimi ni mwendeshaji wa tukutuku. Tukutuku ninayoiendesha ni yangu lakini imezeeka mno. Sikutarajia kuwa mke wangu angejifungua watoto watano. Nilikuwa nikimtarajia mtoto mmoja ni hilo ndilo lilokuwa ombi langu,” alisema kwa hofu. Amesema

Aidha baba huyo mwenye watoto nane ameomba jamii hata serikali imsaidie, kwani kipato chake ni kidogo kulinganisha na ukubwa wa familia aliyonayo.

 

Thomas Tuchel akataa kuwazungumzia Kante, Cavani
Joe Hart kuwekwa sokoni, amtolea uvivu Guardiola

Comments

comments