Mama mzazi wa mwanamitindo nchini Hamisa Mobetto amefunguka mapema jioni hii kuhusu tetesi za kununuliwa nyumba kwa Hamisa Mobeto na kudai kuwa Hamisa hajanunuliwa nyumba.

Mama yake Hamisa amekanusha madai hayo na kusema kuwa nyumba iliyonunuliwa ni ya mjukuu wake Dylan.

Pia amechukua nafasi hiyo kushukuru ujio wa mtoto huyo katika familia yake kwani umekuja na baraka tele zikiwemo za yeye na familia yake kununuliwa nyumba ya ghorofa la bei ghali lililonunuliwa na msanii wa bongo fleva nchini anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki ndani na nje ya nchi, Abdul Naseeb maarufu kama Diamond Platinumz.

”Hamisa hajanunuliwa  nyumba kanunuliwa Dylan ndio mwenye nyumba, kwahiyo namshukuru sana mjukuu wangu kwa kuja kwenye maisha yetu, kwa hiyo  bila Dylani tusingekewa hapa” amesema mama yake Hamisa.

Aidha mama Mobeto amezungumzia swala la Diamond kuoa na kudai kuwa hilo wamwachie Diamond mwenyewe kwani Zari na Hamisa wototo na mama watoto wake.

Na wale amabo wanaomchukia na najua siku moja watakuja kumpenda, wamwache mwanangu waache kumsakama yeye ndio anajua mwanamke gani atakuja kumuoa, nachuoa yule ni mama watoto wake na huyu ni mama mtoto wake

Mama huyo amefunguka hayo mara baada ya kuibuka tetesi zilizodai kuwa Hamisa Mobeto mama mtoto wa Diamond Platinumz amenunuliwa jumba la ghorofa maeneo ya Mbezi Beach mitaa ya Bahari Beach kama ilivyo desturi yake kwa mama mtoto wake.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 13, 2018
Ukifanya haya 7 kila siku utajikinga na magonjwa ya moyo

Comments

comments