Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa ametoa neno baada ya hukumu ya msanii wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu kutolewa, amesema kuwa leo atakwenda makaburi ya kinondonni alipoziikwa mwanaye ili kwenda kumzika upya.

Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji huyo.

“Kwa sasa sina la kusema ila  naishukuru sana Mahakama kwa kutenda haki, pia niishukuru sana Serikali yangu lakini pia nikitoka hapa nitakwenda makaburini kwa ajili ya kumzika upya mwanangu Kanumba”. Mama Kanumba.

Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu, Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake.

Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.

Kigwangala amshambulia Nyalandu, amkabidhisha kwa Takukuru
Bodi ya mikopo yatoa orodha mpya, wanufaika mkopo elimu ya juu