Aliyekuwa mpenzi wa msanii maarufu kutoka nchini Nigeria Davido, aitwaye Sophie Momodu ambaye pia ndiye mama mzazi wa mtoto wa kwanza wa msanii huyo, amewavulia uvivu watu wanaomsumbua kwa kucheza na hisia zake kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii.

Sophie ameonyesha kukasirishwa na kundi la watu linalomuandama kwa kila anachokifanya hasa anapoonekana kumuunga mkono msanii huyo ambaye ni mzazi mwenzie.

Mama mtoto huyo wa Davido alibainisha hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram siku ya Jumatatu, Januari 3, 2022, alipokuwa akijibu tuhuma za kuwa na marumbano na mwanamke ambaye ni mama wa mtoto wa pili wa msanii Davido, ambapo alitajwa kugombana naye kwenye Club ya usiku huko Lagos Nigeria.

Kwa mujibu wa Sophie, anadai ametumia miaka sita iliyopita akipambana na watukutu wa mitandaoni ambao hawajawahi kuona lolote jema kumhusu yeye. Alisema ataendelea kuongea ukweli kwa sababu mtoto wake atakapokuwa mkubwa, atahoji ukimya wake licha ya kuzushiwa habari mbaya na zisizo na ukweli zenye lengo la kumchafua.

Sophie alisema anachojaribu kufanya ni kumlea binti yake vizuri na kuhakikisaha ana uhusiano mzuri na baba yake.

Pia alionyesha kushangazwa na kitendo cha watu wengi kwenye mitandao ya kijamii huko Nigeria, kuonyesha kumshambulia kila anapojaribu kumuunga mkono Davido kwenye jambo lolote.

Amehitimisha kwa kutoa kitisho kuwa ndani ya mwaka huu mpya wa 2022, hatomfumbia macho yeyote, atakayeeneza uvumi juu yake hasa utakaohusu uhusiano uliopo baina yake na mzazi mwenzie.

Sophie na Davido walipata mtoto wao mwaka 2015.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 6, 2022
wanaosababisha migogoro ya ardhi kukiona