Meno ya Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 yamemng’ata mama mtoto wa msanii Nay wa Mitego anayefahamika kwa jina la Siwema, baada ya mahakama jijini Mwanza kumhukumu kifungo cha miaka miwili.

Nay na Siwema

Siwema alihukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kumtukana mtandaoni mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Deo.

Msanii Nay wa Mitego ambaye aliishi muda mrefu na Siwema na kupata mtoto waliyemuita Curtis ameeleza kusikitishwa na mkasa huo uliompata Siwema na kuahidi kufanya kila linalowezekana kuona kinachoweza kufanyika.

“Napambana jinsi ninavyoweza kuona namna ninayoweza kumpa msaada kwa njia yoyote ili asiwe kwenye mazingira ambayo tayari ameshawekwa,” Nay aliiambia Clouds FM na kuongeza kuwa tayari ameshalipata jina la mshtaki wake.

 

WAZIRI MKUU: TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA LAPUNGUA
Lowassa azua tafrani Bungeni, apelekea Bunge kuahirishwa kwa muda