Tarehe 13 Mei kila mwaka duniani kote huwa ni siku ya kina mama ambapo siku hii watu huitumia kuwashukuru mama zao kwa malezi na maisha waliowapa watoto wao.

Katika kuadhimisha siku hii watu wote wakiwemo viongozi, wasanii na watu muhimu katika nchi  hukukiri ushujaa wa mama zao hivyo hutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuandika ujumbe mfupi kwa mama zao.

Hivyo ni vyema upendo huo kwa mama ukadumishwa siku zote.

kupitia ukurasa wa instagram wa msanii mkubwa wa muzuki wa hip hop nchini, Nikki wa Pili ametumia kuukumbusha umma juu ya mama.

”Tumekuumiza kwa uchungu wakati unatuleta duniani, tumekusononesha tulipokuwa tunaugua, tumekuuzi kwa tabia na makosa tulipokuwa tunakua, tumekuchosha zaidi ya miaka 20 ukitutafutia chakula kwa jasho, lakini tunaishia kuhonga na kulizwa na visichana na wakati mwingine tuko karibu na chaja za simu kuliko wewe. Happy Shujaa Day, Happy Mothers Day” amemalizia Niki wa Pili.

Ni dhahili kuwa mtu akishakuwa mtu mzima wa kujitegemea husahau kabisa magumu aliyopitia mama yake wakati wa makuzi yake, wengine huishia kuhonga pesa na husahau kabisa kutuma pesa kwa wazazi wao waliopo kijijini, vijana wengi hutumia muda wao kufanya starehe za maisha na kusahau maisha ya wazazi wao ambao bado huchumia juani.

Leo ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kina mama duniani itumike kuwakumba kina mama wote kwa kuwaonesha unajali, wapo ambao leo hii mama zao walishatangulia mbele za haki na wanatamani wangekwepo, hivyo tumia nafasi yako vizuri mpende, mjali na muheshimu mama yako kwani ndiye Mungu wako wa duniani.

 

 

Ummy afafanua zoezi la kupima Ukimwi bar kwa bar
Picha: Lori lenye ng'ombe 15 waliokufa latelekezwa kwenye machinjio ya Tegeta

Comments

comments