Mke wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Samwel Sitta, Bi Margaret Sitta, leo ameangua kilio bungeni wakati akipokea joho alilokuwa akilivaa marehemu mumewe wakati wa kuongoza vikao vya Bunge.

Hayo yamejiri leo Januari 28, 2020, katika Mkutano wa 18 Kikao cha Kwanza, ambapo amesema kuwa jambo la kuwaenzi viongozi waliowahi kuongoza kiti cha Uspika ni jambo jema na la kihistoria.

“Joho hili daima litaendelea kuwa ni kumbusho la misingi ambayo aliisimamia marehemu, ikiwemo ukweli na uadilifu, kwa niaba ya familia tunawashukuru sana kwa tukio hili la heshima na la kihistoria” amesema Mama Sitta.

Viongozi wengine waliopokea majoho yao ni pamoja na Spika Mstaafu, Pius Msekwa na Mama Anne Makinda.

Anne Makinda atoa wosia mzito kwa wabunge leo, ''Itikadi zisitugawe"
Bulaya arithi mikoba ya Lissu, Spika Ndugai amtangaza

Comments

comments