Mama mzazi wa msanii wa filamu za bongo Irene Uwoya, Neema Mrisho amesema hampendi Dogo Janja kwa sababu msanii huyo hana adabu lakini pia amefunguka na kudai kuwa haitambui ndoa ya mwanaye Irene na Dogo Janja kwani ni ndoa ambayo imefungwa bila kufuata taratibu.

Mama Uwoya amezungumza hayo leo, pindi alipokuwa anajibu hoja ya mwanae Irene aliyedai kuwa hadi leo hajampeleka mume wake nyumbani kutokana na sababu ya kuwa mama yake ni mtu wa kusafiri mara kwa mara hivyo bado wanatafuta muda wa kufanya jambo hilo.

Mama Uwoya amezungumzia utetezi wa mwanaye kuwa hauna mashiko kwani hata kama anasafiri haiwezi kuwa mwaka mzima na kwamba, ukweli ni mtoto wake anajua wazi kuwa ndoa hiyo hawaitambui na hawamkubali Dogo kwa kuwa ni mtoto ambaye hana adabu.

Yaani ndugu mwandishi sijui nisemeje na mambo haya sipendi sana kuyaongea kwenye vyombo vya habari kwa kuwa haipendezi kubishana na mtoto uliyemzaa kwenye vyombo vya habari, kwani mwisho wa siku yule ni mtoto wetu tu pamoja na kufanya mambo ambayo hayajatupendeza lakini mwelewe kwamba ndoa hiyo sisi kama wazazi hatuitambui na hatutaitambua,” amesema mama huyo.

Hata hivyo, mama Uwoya amesema ndoa hiyo ibaki kutambuliwa na hao Irene aliowaita kuwa ni ndugu zake, waliokwenda kushiriki harusi yake na waliomfungisha na kwamba, licha ya wazazi kuwa Dar es Salaam,  wanashangaa walijitokeza ndugu ambao hawawajui kusimamia jambo hilo.

Ameongezea kuwa ”Siku ambayo ndoa inafungwa ndugu zake na wazazi wake tulikuwapo lakini tulishangaa kuona kwenye mitandao kuwa amefunga ndoa na hata ilipozidi kuvuma na kumuuliza majibu yake ilikuwa kwamba, alikuwa anacheza movie hivyo tuliamua kuachana nalo kwa kuwa huwezi kumlazimisha mtu akwambie ukweli kwa kile anachokiamini yeye” Amesema mama Uwoya.

TFF yafafanua kuhusu matumizi ya bilioni 3.7
Real Sociedad yamtimua kocha wake.