Mama wa kijana Ibrahim Abdeslam aliyejitoa mhanga na kujilipua jijini Paris Ufaransa amejitokeza kuzungumzia tukio alilolifanya mwanae.

Mama huyo amemtetea mwanae na kudai kuwa hakuwa na nia ya kumuua mtu yeyote na kwamba bomu alilokuwa amelivaa lilifyatuka bahati mbaya.

Ibrahim Abdeslam mwenye miaka 36, raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Morocco anadaiwa kuwa moja kati ya wasuka mpango wa mashumbulizi sita yaliyosababisha vifo vya watu 229 katika jiji la Paris.

Kijana huyo alijilipua nje ya mgahawa wa Comptoir Voltaire lakini mlipuko wake unasadikika kuwa haukuchukua uhai wa mtu mwingine.

“Huu haukuwa mpango wake, huo ndio uhakika. Ukweli kwamba bomu lake la kujitoa mhanga lililipuka bila kumuua mtu yeyote hali hii inaongea zaidi. Hata tuliweza kumuona siku mbili kabla ya mashambulizi hayo. Hakukua na dalili zozote kuwa kuna mpango wa kufanya vurugu zozote,” alisema mama huyo.

Mama huyo anaongeza kuwa labda bomu hilo lililipuka bila mpango wake huku akidai kuwa huenda mwanae alikuwa na ‘msongo wa mawazo’.

Mama huyo pia alilamikia kitendo cha watoto wake watatu wa kiume kukamatwa na Polisi kufuatia tukio hilo.

Ibrahim alitambulika kama dereva wa gari lililokodiwa muda mfupi kabla ya utekelezaji wa tukio hilo na lilipatikana kwenye eneo la tukio. Gari hilo linadaiwa kuwa lilikuwa limebeba magaidi ambao waliua watu walioenda kupata chakula cha usiku nje ya mgahawa mmoja maarufu.

TFF YATANGAZA TENDA YA MSHAURI WA ELEKTRONIKI
Job Ndugai Achaguliwa Rasmi Kuwa Spika wa Bunge la 11