Mama wa aliyekuwa mpinzani wa Kagame nchini Rwanda amesema kuwa alikuwa akiteswa kipindi akiwa ameweka rumande.

Adeline Rwigara amesema kuwa alipokuwa rumande alikuwa akinyimwa huduma muhimu kama chakula, maji na huduma zingine za kibinadamu kwa muda wa siku tano hivyo imemsababishia matatizo makubwa.

Mama huyo ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu amesema kuwa tuhuma zilizofunguliwa dhidi ya familia yake ni uzushi na kuwa zinatokana na kuikosoa serikali kwa rekodi yake ya uvunjifu wa haki za binadamu.

Aidha, Serikali ya Rwanda ilimuondoa Diane Rwigara katika mchakato wa uchaguzi wa Agosti mwaka huu kwa madai ya kuwa alikuwa hana sifa, hivyo kumfanya Rais Paul Kagame kushinda kwa urahisi.

Hata hivyo, Serikali ya Rais Kagame inatuhumiwa na wanaharakati mbalimbali wa haki za binadamu kuwa inawanyanyasa vyama vya upinzani nchini humo.

LIVE: Rais Magufuli katika maadhimisho ya Nyerere Day na Kilele cha Mwenge wa Uhuru Zanzibar
Hii ndio rekodi ya Lukaku dhidi ya Liverpool