Mwanamitindo wa Marekani Kim Porter ambaye alikuwa mpenzi wa Sean ‘Diddy’ Combs, amekutwa akiwa amefariki, nyumbani kwake Toluca Lake, Los Angeles.

Polisi wa Los Angeles, wametoa taarifa ya uchunguzi wa awali kuwa kifo cha mrembo huyo aliyefariki jana akiwa na umri wa miaka 47 hakikusababishwa na mtu.

Polisi wameeleza kuwa walikuta mwili wake ukiwa umejilaza kitandani, hali inayoonesha kuwa alipoteza maisha akiwa juu ya kitanda hicho.

Kim Porter alikuwa na uhusiano na Diddy kwa kipindi cha miaka 13, tangu mwaka 1994 na walifanikiwa kuzaa watoto watatu.

Diddy alionekana kwenye kipande cha video akiwa nyumbani kwa marehemu, akizungumzana polisi waliofika katika eneo hilo.

Idara ya Polisi ya Los Angeles imeeleza kuwa, “Diddy alikuwa anaonesha ushirikiano wa hali ya juu ingawa alikuwa na majonzi, alipokuwa akizungumza na maafisa wa polisi katika eneo hilo.”

Kwa mujibu wa TMZ, imeelezwa kuwa chanzo cha kifo chake kinaaminika kuwa ni shambulio la moyo.

Kifo chake kimesababisha majonzi katika tasnia ya burudani hasa nchini Marekani. Watu maarufu katika kiwanda cha burudani wametumia mitandao ya kijamii kueleza namna walivyoguswa na kifo hicho.

Mbunge aruka viunzi taarifa za kuhamia CCM
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 16, 2018

Comments

comments