Beki wa kati Mamadou Sakho ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na Liverpool kwa ajili ya michezo ya ligi ya nchini England msimu wa 2016/17.

Beki huyo kutoka nchini Ufaransa, alikua katika harakti za kutaka kuihama kwa mkopo Liverpool kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili usiku wa kuamkia jana, kufuatia utovu wa nidhamu aliouonyesha wakati wa maandalizi ya msimu huko nchini Marekani, lakini dakika za mwisho meneja Jurgen Klopp alibadilisha masimamo wake.

Kabla ya kuonyesha utovu wa nidhamu wakati wa kambi ya maandalizi, Sakho alikua anakabiliwa na kashfa ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini, baada ya kufanyiwa vipimo na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, na matokeo yake alifungiwa kucheza michezo ya mwishoni mwa msimu uliopita.

Hatua ya Jina la beki huyo mwenye umri wa miaka 26 kusajiliwa kwenye kikosi cha Liverpool kitakachocheza ligi kuu msimu huu, inamaanisha uwepo wa maelewano kati yake na Jurgen Klopp ambaye hakuwa na furaha baada ya matukio hayo mawili kujitokea.

Katika hatua nyingine beki Tiago Ilori, naye amejumuishwa katika kikosi cha Liverpool kilichowasilishwa kwenye ofisi za chama cha soka nchini England (FA), baada ya taratibu za kuuzwa kwake kushindikana.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 amekua na wakati mgumu wa kucheza katika kikosi cha kwanza cha Liverpool, kwani mpaka sasa ameshacheza michezo mitatu ya kombe la FA pekee, tangu aliposajiliwa mwaka 2013 akitokea Sporting Lisbon.

Aliwahi kupelekwa kwa mkopo katika klabu za Granada, Bordeaux na Aston Villa.

Danny Ings' playing time has been restricted by injuryDanny Ings

Mshambuliaji Danny Ings, aliyecheza michezo sita pakee tangu alipowasiliwa huko Anfield akitokea Burnley mwezi Juni mwaka 2015, naye ameingizwa kwenye kikosi hicho.

Ifuatayo ni orodha ya wachezaji wanaounda kikosi cha Liverpool ambacho kimesajiliwa kwa ajili ya ushiriki wa michezo ya ligi kuu ya soka nchini England msimu wa 2016/17.

Roberto Firmino Barbosa de Oliveira, Emre Can, Nathaniel Edwin Clyne, Philippe Coutinho Correia, Jordan Brian Henderson, Tiago Ilori, Daniel William John Ings, Loris Karius na Ragnar Klavan

Wengine ni Adam David Lallana, Dejan Lovren, ManeSadio, Alexander Manninger, Job Joel Andre Matip, Simon Mignolet, James Philip Milner, Alberto Moreno Perez, Pezzini Leiva Lucas, Sakho Mamadou, Stewart Kevin Linford, Sturridge Daniel na Wijnaldum Georginio.

Daniel Amoah Aanza Mazoezi Azam FC
Shay Given Kuendelea Kutamba Stoke City